Sinopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodios
-
Matukio makubwa ya kisiasa yaliyotikisa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2025
31/12/2025 Duración: 10minMatukio makubwa ya kisiasa tuliyochambua mwaka 2025 ni pamoja na kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya Raila Odinga, uchaguzi wenye vurugu uliofanyika nchini Tanzania Oktoba 29 na kutiwa saini kwa mkataba wa kumaliza vita Mashariki mwa DRC, Desemba 04, jijini Washington DC nchini Marekani.
-
DRC: Kuondoka kwa waasi wa M23/AFC mjini Uvira kunamaanisha nini ?
24/12/2025 Duración: 09minBaada ya shinikizo kutoka kwa Marekani, waasi wa M23/AFC waliondoka kwenye mji wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivyo, rais Felix Tshisekedi ameelezea kitendo hicho kama kiini macho kwa jumuiya ya Kimataifa, kauli ambayo imeungwa na mkono na jeshi la FARDC wanaosema, waasi hao wamejificha katika milima inayopatikana na mji huo. Kuchambua kinachoendelea, tunaungana Mali Ali akiwa jijini Paris na François Alwende akiwa jijini Nairobi.
-
DRC: Nini hatima ya Uvira baada ya M23/AFC kuuteka mji huo ?
17/12/2025 Duración: 10minHali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, si shwari licha ya kutiwa saini kwa mkataba unaolenga kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka 30. Waasi wa M23/AFC wameudhibiti mji wa Uvira. Marekani inaonya kuichukulia hatua Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao ambao sasa wameahidi kuondoa vikosi vyake katika mji huo, lakini kwa masharti. Tunachambua kwa kina.
-
Wanasiasa wa upinzani kukabiliwa na vurugu, Uganda
10/12/2025 Duración: 10minKampeni za uchaguzi nchini Uganda zimezidi kupamba moto kuelekea uchaguzi mkuu January 15 2025 ambapo Rais Yoweri Museveni aliyeingia madarakani mwaka wa 1986, anagombea tena muhula wa saba huku akishindana na wagombea wengine miongoni mwao mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine. Kampeni za mwaka huu zinafanyika huku mgombea wa Upinzani Bobi wine akilalamika kushambuliwa na maafisa wa usalama. Kupata mengi zaidi ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
-
Viongozi wa DRC na Rwanda kutia saini makubaliano ya amani, huko Washington DC
03/12/2025 Duración: 10minMakala ya wimbi la siasa, imeangazia hatua ya viongozi wa Rwanda na DRC ambao siku ya alhamisi desemba 04 watatia saini makubaliano ya amani, mbele ya rais wa Marekani Donald Trump hii ikiwa ni mwendelezo wa mapatano ya amani mashariki mwa DRC yaliyosimamiwa na Marekani yaliyotiwa saini na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili juni 27. Profesa Pacifique Malonga ni mchambuzi wa siasa akiwa Kigali Rwanda, pia Francois Alwende ni mtaalamu wa siasa za maziwa makuu akiwa Nairobi Kenya.
-
Oburu, atafanikiwa kukiunganisha chama ODM kuelekea uchaguzi mkuu 2027 ?
19/11/2025 Duración: 10minChama kikuu cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement-ODM kina kiongozi mpya, Seneta Oburu Oginga, kaka yake kiongozi wa zamani wa chama hicho Hayati Raila Odinga aliyefariki dunia mwezi Oktoba. Je, atafanyaje, kukiunganisha chama hicho ambacho kinaonekana kugawanyika kuhusu ushirikiano wake na uongozi wa rais William Ruto ? Tunachambua.
-
Nini suluhu ya utekaji wa watu katika nchi za Afrika Mashariki ?
12/11/2025 Duración: 10minNchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania, zimeendelea kushuhudia ongezeko la visa vya wakosoaji wa serikali kutekwa na kupotezwa. Hivi karibuni, wanaharakati wawili kutoka nchini Kenya, Bob Njagi na Nicholas Oyoo walitekwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita nchini Uganda, baada ya kuhudhuria kampeni za uchaguzi za Bobi Wine, waliachiwa baada ya shinikizo za watetezi wa haki za binadamu. Nani atakomesha utekaji ?
-
Nini hatima ya Tanzania baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu ?
05/11/2025 Duración: 10minMachafuko yalikumba uchaguzi mkuu wa Tanzania, uliofanyika Oktoba 29, 2025 na rais Samia Suluhu Hassan kutangazwa mshindi kwa kupata asilimia 97.6 ya kura. Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimesema ushindi wa Samia ni kichekesho cha demokrasia. Anapaswa kufanya nini ili kuirejesha Tanzania katika utulivu wa kisiasa ? Tunachambua.
-
Watanzania wapiga kura bila uwepo wa upinzani
29/10/2025 Duración: 10minWatanzania wanapiga kura kuwachagua wabunge, madiwani na rais, katika uchaguzi ambao rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuibuka mshindi, baada ya mpinzani wake mkuu Tundu Lissu, kuzuiwa jela na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
-
DR Congo: Kabila akutana na wanasiasa wa upinzani jijini Nairobi
15/10/2025 Duración: 10minRais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, anakutana na wanasiasa wa upinzani jijini Nairobi, kuanzia Oktoba 14, wiki mbili baada ya kuhukumiwa kifo na Mahakama ya kijeshi. Wanasiasa hao wanazungumza nini ? Tunachambua.
-
Uchambuzi: Kwanini waasi wa AFC/M23 waendelea kujiimarisha zaidi mashariki mwa DRC ?
08/10/2025 Duración: 10minWachambuzi wa mambo wanaona kuwa waasi wa AFC/M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi, katika maeneo wanayodhibiti, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa Washington uliokubaliwa kati ya DRC na Rwanda kuhusu namna ya kupata mwafaka wa kudumu. Hatua hii inamaanisha nini ? Tunachambua.
-
Rais Museveni kuchuana tena na Bobi Wine kwenye uchaguzi wa urais 2026
01/10/2025 Duración: 10minKampeni za uchaguzi mkuu nchini Uganda, uliopangwa kufanyika Januari 12, 2026, zilianza Septemba 29. Kuna wagombea wanane wa urais, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 39. Mpinzani wake mkuu ni Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 43. Nini kinachotarajiwa kwenye kampeni hizi ?
-
DR Congo: Nini hatima ya Kamerhe, baada ya kujiuzulu Uspika ?
24/09/2025 Duración: 10minVital Kamerhe, Septemba 22, alijiuzulu kama Spika wa Bunge la taifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kuundwa kwa Tume ya kumchunguza dhidi ya madai ya matumizi mabaya ya madaraka, kuwahangaisha wabunge na kuwalazimisha kupitisha miswada haraka haraka.Nini hatima ya kisiasa ya Kamerhe baada ya kujiuzulu ? Ataendeleza ushirikiano wake wa karibu na rais Felix Tshisekedi ?
-
Nini hatima ya Sudan Kusini baada ya Machar kufunguliwa mashtaka ya uhaini ?
17/09/2025 Duración: 10minNchini Sudan Kusini, serikali ya rais Salva Kiir, imetangaza kumfungulia mashtaka ya uhaini na uhalifu wa kivita, kiongozi wa upinzani Riek Machar, ambaye ameondolewa kwenye nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais, kufuatia shambulio la wapiganaji wa White Army kwenye kambi ya jeshi katika jimbo la Upper Nile mwezi Machi mwaka 2025. Nini hatima ya Machar na Sudan Kusini ?
-
Kwanini wakaazi wa Uvira hawamtaki Jenerali Olivier Gasita ?
10/09/2025 Duración: 10minMji wa Uvira, jimboni Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa zaidi ya wiki moja, ikiwemo Septemba 08, umeshuhudia maandamano yaliyopangwa na mashirika ya kiraia na wapiganaji wa Wazalendo, kupinga kupinga kuteuliwa kwa Jenerali Olivier Gasita, kuwa Naibu Kamanda wa Kikosi cha jeshi la FARDC, katika eneo hilo kwa madai ya kuwa na ushirikiano na waasi wa AFC/M23 kwa sababu ya kabila lake la Banyamulenge.
-
Tanzania yaingia kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu
27/08/2025 Duración: 10minTanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu kuanzia Agosti 28, kuelekea kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025. Rais Samia Suluhu Hassan, kutoka chama tawala CCM, anawania uongozi wa nchi hiyo. Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.
-
Trump atafanikiwa kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine ?
20/08/2025 Duración: 10minRais wa Marekani Donald Trump, amechukua hatua ya kuongoza harakati za kumaliza vita vya miaka mitatu vya Urusi nchini Ukraine. Trump amekutana na rais Vladimir Putin na Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine pamoja na viongozi wengine wa nchi za Ulaya Agosti 18, baada ya awali kukutana na rais Putin Agosti 15 jimboni Alaska. Je, Trump atafanikiwa kumaliza vita hivyo ?
-
Serikali ya DRC na waasi wa M23/AFC wakubaliana kumaliza vita
23/07/2025 Duración: 10minJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23/AFC, Julai 19, walitia saini rasimu ya makubaliano jijini Doha nchini Qatar ya namna ya kusitisha vita Mashariki mwa DRC na kupata amani ya kudumu. Ni mambo yepi yaliyokubaliwa na changamoto zipi zinazokabili pande hizi mbili kwenye utekelezwaji ? Tunajadili.
-
Rais Museveni ateuliwa tena kuwania urais nchini Uganda
16/07/2025 Duración: 10minKiongozi wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80, ameteuliwa na chama chake cha NRM, kugombea tena urais wakati wa uchaguzi mkuu uliopagwa kufanyika mapema mwaka 2026, baada ya kuwa madarakani miaka 40. Hii inamaanisha nini katika siasa za Uganda ?
-
Kwanini vijana wa Gen Z wanaendelea na maandamano nchini Kenya ?
09/07/2025 Duración: 10minVijana nchini Kenya maarufu kama Gen Z, wameendelea kuandamana dhidi ya serikali ya rais William Ruto. Maandamano haya yameishia kwenye maafa na majeruhi tangu mwezi Juni mwaka 2024. Tunaungana na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha NIBS kilichopo Ruiru, kusikia kutoka kwao. Kwanini wanaandamana ?