Wimbi La Siasa

DRC: Kuondoka kwa waasi wa M23/AFC mjini Uvira kunamaanisha nini ?

Informações:

Sinopsis

Baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani, waasi wa M23/AFC waliondoka kwenye mji wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivyo, rais Felix Tshisekedi ameelezea kitendo hicho kama kiini macho kwa jumuiya ya Kimataifa, kauli ambayo imeungwa na mkono na jeshi la FARDC wanaosema, waasi hao wamejificha katika milima inayopatikana na mji huo. Kuchambua kinachoendelea, tunaungana  Mali Ali akiwa  jijini Paris na François Alwende akiwa jijini Nairobi.