Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:24:26
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Simulizi za mateso na matumaini ya wakimbizi wa muda mrefu katika makazi ya wakimbizi ya Kiryandongo Uganda

    16/04/2026 Duración: 05min

    Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani. Kwa Afrika ni ya kwanza ikihifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Burundi, rwanda, Sudan, Sudan Kusini na hata Kenya. Katika mada kwa kina hii tunaangazia wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi. Abdelmonem Makki wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni ameyatembelea makazi hayo na kuzungumza na wakimbizi hao kutoka Sudan. Na sasa kwa lugha ya Kiswahili, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anasimulia.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU”

    16/04/2026 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” 

  • 16 APRILI 2026

    16/04/2026 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazw

  • UNDP yasaini makubaliano kuwezesha wanawake wasanifu majenzi Tanzania

    15/04/2026 Duración: 03min

    Katika kuunga mkono lengo namba 9 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kuhusu miundombinu na ujenzi wenye mnepo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania, limeingia makubaliano ya kimkakati na Taasisi ya wanawake wasanifu Majenzi, TAWAH, kwa ajili ya kuboresha sekta ya ujenzi. Makubaliano hayo yaliyowekwa saini Aprili 8, 2026, yanalenga kutambua madini ya ujenzi na viwandani yaliyosahaulika, kukuza ujenzi usioharibu mazingira na kuwawezesha wanawake kiuchumi. Rashid Malekela na taarifa zaidi.

  • Miaka mitatu ya vita nchini Sudan madhila kwa raia ni jinamizi linaloendelea: UN

    15/04/2026 Duración: 03min

    Leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini Sudan 15 Aprili 2023, mgogoro ambao umegeuka kuwa moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Mamilioni ya watu wamekwama katikati ya mapigano, kuwa wakimbizi wa ndani na nje, njaa na ukosefu wa makazi, huku mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yakionya kuwa mateso yanaendelea kuongezeka kila uchao. Flora Nducha na taarifa zaidi

  • 15 APRILI 2026

    15/04/2026 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za Umoja wa Mataifa za kutafuta suluhu ya vita nchini Sudan pamoja na simulizi za wakimbizi ikiwa leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini humo, na miundombinu na ujenzi wenye mnepo nchini Tanzania.Wakati vita nchini Sudan ikiingia mwaka wa nne tangu kuvuka kwa mapigano baina ya jeshi la Sudan na kikosi vya msaada wa haraka RSF, hii leo huko Berlin nchini Ujerumani unafanyika mkutano wa Kimataifa ukilenga kurejesha mgogoro wa Sudan katika ajenda ya juu ya kidiplomasia duniani.Leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini Sudan 15 Aprili 2023, mgogoro ambao umegeuka kuwa moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Mamilioni ya watu wamekwama katikati ya mapigano, kuwa wakimbizi wa ndani na nje, njaa na ukosefu wa makazi, huku mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yakionya kuwa mateso yanaendelea kuongezeka kila uchao.Katika kuunga mkono lengo namba 9 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kuhusu miundombinu na ujenzi wenye mnepo, Shirika

  • Wanadiplomasia wanakutana kusaka suluhu ya vita Sudan ikiingia mwaka wa 4

    15/04/2026 Duración: 03min

    Wakati vita nchini Sudan ikiingia mwaka wa nne tangu kuvuka kwa mapigano baina ya jeshi la Sudan na kikosi vya msaada wa haraka RSF, hii leo huko Berlin nchini Ujerumani unafanyika mkutano wa Kimataifa ukilenga kurejesha mgogoro wa Sudan katika ajenda ya juu ya kidiplomasia duniani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mush

  • Jifunze Kishwahili: Maana za neno "KUDA"

    14/04/2026 Duración: 59s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUDA"

  • 14 APRILI 2026

    14/04/2026 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Waziri wa sheria na ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Emmanuel Ugirashebuja amezungumza na Idhaa hii na anaeleza siri ya wananchi wa Rwanda kuweza kuishi kwa amani baada ya mauaji hayo.Kama mapigano yataendelea nchini Sudan hadi mwaka 2030, umaskini wa kupindukia unaweza kuongezeka na kuvuka asilimia 60, huku watu wengine milioni 34 wakitumbukia kwenye ufukara, imesema Ripoti ya uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliyotolewa leo Sudan na Marekani ikiwa kesho inatimia miaka mitatu kamili tangu kuanza kwa vita.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa kauli zao tofauti tofauti kuhusu miaka mitatu ya vita nchini Sudan ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto wanaendelea kulipa gharama ya vita kwani zaidi ya watoto 245 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu Januari hadi Machi mwaka huu, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani au droni yamesababi

  • Kuvurugika kwa meli kupita mlango bahari wa Hormuz kunazua wasiwasi kuhusu bei za chakula na minyororo ya usambazaji duniani

    13/04/2026 Duración: 03min

    Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

  • UNMISS yaimarisha ulinzi wa amani Sudan Kusini kwa ukarabati wa barabara Malakal

    13/04/2026 Duración: 03min

    Kufuatia mafuriko makubwa yanayoendelea kuharibu miundombinu na kukwamisha ulinzi wa amani huko  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS unaendelea kujitahidi kukarabati miundombinu kama njia mojawapo ya kuongeza ustahimilivu na kuchochea amani. Feissal Kirwa amefuatilia kutuandalia taarifa hii.

  • 13 APRILI 2026

    13/04/2026 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mlango Bahari wa Hormuz, mafuriko na ukarabati wa miundombinu huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, na juhudi za FAO nchini Tanzania za kuwapatia mafunzo jamii kuhusu lishe bora.Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani.Kufuatia mafuriko makubwa yanayoendelea kuharibu miundombinu na kukwamisha ulinzi wa amani huko  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS unaendelea kujitahidi kukarabati miundombinu kama njia mojawapo ya kuongeza ustahimilivu na kuchochea amani.Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakul

  • FAO nchini Tanzania yapatia wakazi wa Kigoma mafunzo ya vitendo kuhusu lishe bora

    13/04/2026 Duración: 03min

    Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), maafisa ugani wa kilimo, wataalamu wa lishe na afya mkoani Kigoma waliungana kuandaa tukio la Siku ya Afya na Lishe Mitaani au SALIMI sambamba na Siku ya Shamba la Mkulima ili kuwapatia wakulima na wanajamii elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji na matumizi ya mazao yenye lishe. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

  • UN: Kuanzia Lebanon hadi Sudan kote ni simulizi ya giza la vita na kukimbia makazi

    10/04/2026 Duración: 02min

    Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan. 

  • Mwanafunzi Ahmad Omar aongoza mabadiliko ya kijani shule ya Kisiwandui Zanzibar

    10/04/2026 Duración: 02min

    Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko haya.

  • 10 APRILI 2026

    10/04/2026 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea nchini Sudan, juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya, na kazi za wanafunzi katika utunzaji wa mazingira huko Zanzibar.Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan.Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi ki

  • Ukatili wa Kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya waibua wadau, viongozi - UNFPA

    10/04/2026 Duración: 02min

    Baada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Leah Mushi na taarifa zaidi.

  • 09 APRILI 2026

    09/04/2026 Duración: 09min

    Jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa CSW70 akieleza ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya Lebanon tarehe 8 Aprili, mashambulizi ambayo yamesababisha mamia ya raia kuuawa na kujeruhiwa, wakiwemo watoto, sambamba na kuharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya kiraia. Taarifa iliyotolewa New York, Marekani na Msemaji wa Umoja wa Mataifa inamnukuu Guterres akionesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la vifo miongoni mwa raia na kutoa pole kwa watu na Serikali ya Lebanon, akiwatakia nafuu ya haraka wale waliojeruhiwa.Katika tukio jingine hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezindua Mfuko wa Urejeshaji wa Palestina uliopewa jina la Horizon Fund, akisisitiza um

  • UNICEF na Benki ya Dunia warejesha matumaini ya elimu kwa watoto nchini Sudan kupitia programu mbadala za kujifunza

    08/04/2026 Duración: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.

  • Huduma za afya ziko ukingoni kuporomoka kabisa huko Gaza kuliko wakati mwingine wowote

    08/04/2026 Duración: 02min

    Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

página 1 de 5