Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:04:37
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episodios

  • Rais Tshisekedi asema katiba ya Congo itarekebishwa, kesi ya naibu rais wa Kenya

    26/10/2024 Duración: 20min

    Kauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

  • Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda

    19/10/2024 Duración: 20min

    Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

  • Mchakato wa kuondolewa madarakani naibu rais wa Kenya, mazishi ya waliokufa Goma

    12/10/2024 Duración: 20min

    Wabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi

  • Mswada wa kumwondoa naibu rais wa Kenya Kachagua, watu zaidi 78 wafamaji DRC

    05/10/2024 Duración: 20min

    Makala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli  na mambo mengine.

  • Lisu kuishitaki Tanzania kwa jaribio la kumuua, Kenya kupeleka polisi Haiti

    28/09/2024 Duración: 20min

    Mwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan,  siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.

  • Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wanadiplomasia, msamaha kwa mkuu wa polisi Kenya

    21/09/2024 Duración: 20min

    Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.

  • Uchunguzi wa miili ya wanafunzi waliokufa Kenya, hali ngumu ya wakimbizi DRC na mengineyo

    14/09/2024 Duración: 20min

    Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.

  • Mkutano wa 9 China na Afrika, miili200 yazikwa DRC, wanafunzi 17 wateketea Kenya.

    07/09/2024 Duración: 20min

    Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.

  • Kampeni ya Odinga kuwania uenyekiti tume ya AU, DRC yafungua kesi dhidi ya Rwanda

    31/08/2024 Duración: 20min

    Uzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba

  • DRC yaathirika na M-Pox, Raila asema siasa za Kenya, basi! na mengineyo

    24/08/2024 Duración: 20min

    Tumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais  Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo

  • Mpox yatangazwa janga la kimataifa la kiafya, mwanahabari wa Burundi Irangabiye aachiwa na mengineyo

    20/08/2024 Duración: 20min

    Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.

  • Tshisekedi amshutumu mtangulizi wake Kabila, serikali mpya Kenya na mengineyo

    10/08/2024 Duración: 20min

    Makala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani. 

  • Hamas yalaani mauaji ya kiongozi wake, mauaji ya kimbari DRC Genocost, na mengineyo

    03/08/2024 Duración: 20min

    Makala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh  nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.

  • Michezo ya olimpiki yaanza Paris Ufaransa, Siasa za Kenya, DRC na kwengineko

    27/07/2024 Duración: 20min

    Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris  akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.

  • Ruto ateua mawaziri wapya, Paul Kagame ashinda uchaguzi, usalama bado mashariki DRC

    20/07/2024 Duración: 20min

    Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-  

  • Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC

    13/07/2024 Duración: 20min

    Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.  

  • DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwa

    06/07/2024 Duración: 20min

    Miongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.

  • Ruto asema hatasaini mswada wa fedha 2024, M23 wauteka mji wa Kanyabayonga

    29/06/2024 Duración: 20min

    Makala hii imeangazia maandamano nchini Kenya huku rais Ruto akisema hatasaini mswada wa fedha wa 2024 uliokuwa umeidhinishwa na wabunge walio wengi, waasi wa M23 huko DRC walifanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wilayani Lubero mashariki mwa DRC, mgomo wa wafanyabiashara nchini Tanzania, na nini hatima yake, siasa za Afrika kusini lakini pia  mdahalo kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Joe Biden kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, yaliyojiri nchini Ufaransa na kwengineko Duniani.

  • Maandamano nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024, hali ya usalama DRC

    22/06/2024 Duración: 20min

    Makala imeangazia hatua ya wabunge wa Kenya kuidhinisha mswada wa fedha wa 2024 kuingia katika hatua ya pili kabla ya kupitishwa licha ya maandamano makubwa nchini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Lubumbashi, na kuendelea kwa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23, Uganda yawasamehe waasi wa zamani wa ADF, kuapishwa kwa rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, hali huko Afrika Magharibi, na kwengineko duniani

  • Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti, serikali mpya DRC yazinduliwa

    15/06/2024 Duración: 20min

    Tunayoangazia ni pamoja na kutangazwa kwa badgeti ya mwaka 2024/2024 kwenye nchi za jumuia ya Afrika mashariki, serikali ya mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu mpya huko DRC ilizinduliwa wiki hii, mauaji ya ADF huko Lubero mashariki mwa nchi hiyo, kifo cha makamu rais wa Malawi katika ajali ya ndege, lakini tutaangazia yaliyojiri Afrika Magharibi, kabla ya kuelekea kwengineko duniani

página 1 de 2