Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
KILA SIKU YA IJUMAA KWENYE KPINDI CHA HABARI RAFIKI NI MADA HURU
24/10/2025 Duración: 10minLeo ni siku ya mada huru. Tunakupa nafasi kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii Unaweza pia kujadili kile ambacho umekisikia katika matangazo yetu ya wiki hii kwenye redio.
-
WANASAYANSI VIONGOZI WAKUTANA AFRIKA KUSINI KUJADILI AFYA BILA UFADHILI WA NJE
23/10/2025 Duración: 10minViongozi wa dunia, wataalam wa Afya na wanasayansi wanakutana Afrika Kusini siku chache kabla kikao cha G20, ili kuanganzia kuhusu njia za kufadhili afya bila kutegemea ufadhili wa kigeni.Tumemuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu uwezo wa mataifa ya Afrika kufadhili miradi ya afya?
-
Mateka wa Israeli waliokuwa wanashikiliwa na Hamas waachiwa huru huko Gaza
13/10/2025 Duración: 10minHivi leo viongozi wa dunia akiwemo rais wa Marekani, Donald Trump, wanakutana Misri kujadili mustakabali wa eneo la Gaza, baada ya makubaliano ya kihistoria ya wiki iliyopita. Makubaliano haya yameshuhudia kuachiwa kwa mateka, wafungwa na kusitishwa kwa vita vya Gaza. Tunakuuliza, unaamini makubaliano kati ya Hamas na Israel safari hii yatadumu?Nini cha zaidi kifanyike?Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
-
Tuzo ya nobeli kutolewa ijumaa wiki hii
09/10/2025 Duración: 09minMsikilizaji kesho Ijumaa oktoba 10 kamati inayotoa tuzo za kimataifa za Nobel itamtangaza mshindi, wakati huu watu wengi wakiwa wamempendekeza rais wa Marekani Donald Trump kutokana na mchango wake wa kutafuta amani mashariki ya kati, hata hivyo wadadisi wanasema kiongozi huyo hawezi kupewa tuzo hiyo. Unafikiri ni Kiongozi gani anastahili kupewa tuzo hii mwaka huu na kwanini? Ungana nami Ruben Lukumbuka, mubashara kutoka studio namba mbili hapa karibu tuandamane hadi tamati.-