Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:29:02
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • CHAN 2024: Kenya, DRC, Morocco zafukuzia ushindi mechi za mwisho za makundi

    16/08/2025 Duración: 21min

    Leo tumekuandalia uchambuzi wa timu ambazo zimefuzu, gani zimeondolewa na nani wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Chan, michuano ya baskeboli ya wanaume ya Afrika, viongozi wa mashabiki Sudan Kusini waandaa mechi ya kirafiki kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, rais wa AS Kigali aahidi kuongeza tuzo za ligi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa shirikisho, Alcaraz afuzu robo fainali michuano ya Cincinnati Open.

  • CHAN 2024: Kenya yafukuzia ushindi dhidi ya Morocco, Tanzania ikihitaji sare tu

    09/08/2025 Duración: 23min

    Leo tumekuandalia uchambuzi, matokeo na matukio ya raundi ya pili ya hatua ya makundi ya michuano ya CHAN pamoja na mechi za leo usiku na kesho mchana, droo ya michuano ya awali ya kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa barani Afrika, uhamisho wa wachezaji Afrika Mashariki huku Kinshasa ikichaguliwa kuandaa mkutano mkuu wa CAF mwezi Oktoba, Thomas Partey kujiunga na Villareal licha ya kesi za ubakaji, 

  • CHAN 2024: Tanzania na Kenya zashinda mechi zao za kwanza za makundi

    03/08/2025 Duración: 23min

    Tunaendelea kuangazia michuano ya CHAN ambapo wenyeji Kenya na Tanzania wasajili ushindi mechi zao za kwanza, Sudan Kusini yabanduliwa kwenye hatua ya nusu fainali michuano ya basketboli ya kina dada ya Afrobasket, bondia Patrick Mukala wa DRC ndiye bingwa mpya wa Afrika uzani wa light heavyweight, Hojlund wa Man Utd awekewa dau la pauni milioni 30 kuuzwa, matokeo ya hatua ya tisa ya Tour du France na Formula One mkondo wa Hungarian Grand Prix

  • CHAN 2024: Tanzania na Burkina Faso kufungua mashindano ya Chan leo usiku

    02/08/2025 Duración: 23min

    Tumekuandalia mengi leo ikiwemo kuanza kwa mashindano ya CHAN - uchambuzi, matukio na matokeo, michuano ya basketboli ya wanawake yaingia nusu fainali, Gor Mahia yapata benchi mpya la ufundi huku shirikisho la soka nchini Kenya likipata mdhamini mpya wa ligi, tetesi za uhamisho ulaya, matokeo ya hatua ya tatu ya Canada Open, Barcelona yaingia kwenye udhamini wa jewi na taifa la DRC

página 2 de 2