Sinopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodios
-
Dunia: watoto wanazidi kutumika kama vijakazi
23/08/2025 Duración: 10minMwezi wa Juni ulishuhudia matukio mawili muhimu ya kimataifa yakiangazia haki na ustawi wa watoto. Mnamo tarehe 12 Juni, dunia iliadhimisha Siku ya kupinga Ajira ya Watoto, (World Day Against Child Labor) ikirejelea takwimu za kutisha kwamba watoto milioni 160 duniani kote bado wamenaswa katika ajira ya watoto - wengi wakifanya kazi chini ya mazingira hatarishi. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Africa : Mazingira yanavyoathiri haki za watoto
22/08/2025 Duración: 09minKatika makala haya tunangazia uharibifu wa mazingira unavyoathiri haki za watoto. Skiza makala haya kufahamu zaidi.
-
Kenya : Haki ya kumiliki ardhi ya jamii ya wafugaji
22/08/2025 Duración: 10minJamii za wafugaji nchini Kenya, bado zinapitia changamoto za kumiliki ardhi, jamii hizo ni kama vile,Turkana, Samburu, Rendille, Borana, Gabra na nyingine , zimeathiriwa kwa muda mrefu na unyang’anyi wa ardhi wakati wa ukoloni, ambao uliendelezwa hata baada ya uhuru . Licha ya kutambuliwa kwa haki za jamii katika Katiba ya 2010 na kupitishwa kwa Sheria ya Ardhi ya Jamii ya mwaka 2016, jamii hizi bado zinakumbwa na changamoto za ardhi,unyang’anyaji wa mashamba na ukosefu wa haki za kisheria—hali inayotishia siyo tu maisha yao bali pia utamaduni.
-
EAC : Uhuru na haki ya wanahabari kujiunga miungano
30/07/2025 Duración: 09minKataika makala haya tunajadili umuhimu wa wanahabari kuelewa na kulinda haki zao, hasa kupitia vyama na miungano ya waandishi wa habari. Katika mazingira ambapo uhuru wa habari uko mashakani, na waandishi wengi wanakumbwa na changamoto kazini, je, kuna msaada wowote wa pamoja? Ni moja tu ya maswali tunayatarajia kuyajibu kwenye makala ya haya. Skiza makala haya kufahamu mengi