Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 134:18:54
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodios

  • Mkutano wa COP30 umekamilika na makubaliano yamefikiwa

    25/11/2025 Duración: 07min

    Wajumbe wa mkutano wa COP30 nchini Brazili wamefikia makubaliano ya kushughulikia ongezeko la uzalishaji wa gesi duniani. Makubaliano hayo yanaongeza fedha kwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini hayana mpango maalum kuhusu mafuta ya kisukuku.

  • Australia yafafanuliwa:Tamasha ya muziki na utamaduni wa Afrika

    25/11/2025 Duración: 06min

    Wikendi iliyopita, jiji la Melbourne liliendelea kungara kwa rangi, muziki na Ladha za barani Afrika wakati wa tamasha la utamaduni wa afrika lililowajumuisha watu kutoka mataifa mbali mbali. Tamasha hilo lililoandaliwa Federation square, liliwaleta Pamoja maelfu ya wakaazi wa Melbourne na wageni kutoka majimbo tofauti, wote wakikusanyika kusherehekea urithi na utambulisho wa Kiafrika.

  • Australia yafafanuliwa: wanafunzi wa kimataifa waonywa dhidi ya utapeli

    25/11/2025 Duración: 04min

    Onyo la dharura limetolewa kwa wanafunzi wa kimataifa wanaoondoka Australia wasiuze akaunti zao za benki na vitambulisho kwa wahalifu. Polisi ya Shirikisho ya Australia inasema kwamba wanafunzi wanapewa 'pesa ya haraka' - lakini kukubali ofa kama hiyo kunaweza kuwahusisha milele na mitandao ya uhalifu.

  • Australia yafafanuliwa:Afya ya akili katika ujauzito na baada ya kujifungua

    24/11/2025 Duración: 09min

    Karibu mmoja kati ya Waustralia wanne hawatafuti msaada wanapopata matatizo ya afya ya akili wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua. Wataalamu wanasema kwamba taarifa zilizotolewa na Gidget Foundation zinaonyesha ukosefu wa kuelewa dalili na ishara, pamoja na unyanyapaa unaoendelea kuhusu suala hili.

  • Taarifa ya habari tarehe 21 Novemba

    21/11/2025 Duración: 11min

    Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

  • Taarifa ya habari tarehe 18 Novemba

    21/11/2025 Duración: 10min

    Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

  • Taarifa ya habari tarehe 14 Novemba

    21/11/2025 Duración: 10min

    Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

  • Taarifa ya habari tarehe 11 Novemba

    21/11/2025 Duración: 12min

    Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

  • Yaliyojiri Afrika 21 Novemba

    21/11/2025 Duración: 08min

    Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

  • Yaliyojiri Afrika 18 Novemba

    21/11/2025 Duración: 08min

    Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

  • Yaliyojiri Afrika 14 Novemba

    21/11/2025 Duración: 06min

    Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

  • Yaliyojiri Afrika 11 Novemba

    21/11/2025 Duración: 06min

    Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

  • Yaliyojiri Afrika 7 novemba

    21/11/2025 Duración: 07min

    Jason Nyakundi anatujuza yanayojiri Afrika.

  • Tahadhari kwa wanaohitimu shule

    21/11/2025 Duración: 04min

    Kadri maelfu ya vijana wanaposherehekea kumaliza Mwaka wa 12, wanakumbushwa juu ya hatari zinazokuja na unywaji pombe, hasa nje ya nchi. Wazazi na marafiki wa waathiriwa wa sumu ya methanol, Bianca Jones na Holly Bowles, wamejiunga na juhudi mpya za usalama, wakiwatia moyo wasafiri vijana kuchukua maamuzi salama zaidi.

  • Programu za kufunza watu wazima kusoma na kuandika

    21/11/2025 Duración: 05min

    Mmoja kati ya Waaustralia watano, au takriban watu wazima milioni tatu, wana kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na kuandika au hesabu - na hii inaweza kuwa na athari kubwa katika jinsi watu wanavyoweza kushiriki maisha ya kila siku. Programu zimewekwa kote nchini kusaidia watu kuboresha ujuzi wao na kufikia malengo yao ya maisha. Ikiwemo moja huko Tasmania, ikiwasaidia watu wazima kuwa tayari kwa kazi.

  • Watu wa asili kwenye hatihati ya kutoweka Brazil

    18/11/2025 Duración: 08min

    Shirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.

  • Uzalishaji wa Net Zero nchini Australia

    18/11/2025 Duración: 08min

    Muungano umeidhinisha rasmi kuondoa lengo la kutofikia uzalishaji wa gesi chafu katika mkutano wa chumba cha chama huko Canberra. Zaidi ya hayo, Liberals na Nationals wamefunua mpango wa kuondoa mabadiliko ya tabianchi kutoka kwenye orodha ya malengo ya mdhibiti wa nishati ya kitaifa, huku wakiapa kuendelea kupunguza uzalishaji kwa kufuatilia maendeleo ya nchi nyingine.

  • Maumivu ya wanawake kutiliwa maanani zaidi

    14/11/2025 Duración: 08min

    Serikali ya Victoria imetoa ripoti ya mwisho ya uchunguzi kuhusiana na uzoefu wa wanawake katika suala la maumivu - na ni taarifa inayosumbua kusoma. kutokana na uzoefu wa wanawake na wasichana 13,000, ripoti hiyo imebaini mapengo katika huduma za afya kwa jinsia, upendeleo katika matibabu, ubaguzi wa kijinsia, na hisia za kupuuzwa au kutopingwa na wataalamu wa afya zinazoenea katika mfumo wa afya wa Victoria.

  • Maandamano ya kikundi cha NSN uliwezaje kuruhusiwa kufanyika

    14/11/2025 Duración: 08min

    Maandamano ya neo-Nazi mbele ya bunge la New South Wales yamezua mshtuko katika jamii za Kiyahudi na za tamaduni mbalimbali huko Sydney. Serikali ya jimbo hilo imekashifiwa baada ya kufichuliwa kwamba tukio hilo liliendelea na idhini kutoka kwa Polisi wa New South Wales. Je, ni vipi maandamano haya ya neo-Nazi yalipewa kibali cha kufanyika mwanzoni?

  • Mazungumzo kuhusu African Youth Summit 2025

    14/11/2025 Duración: 11min

    Mkutano wa kwanza wa African Youth Summit uliandaliwa na kufanyika mwaka huu, na mratibu wa vijana aliyehudhuria anajiunga nasi kuzungumzia mada ya mkutano huo.

página 3 de 34